Tuesday, 1 May 2018

MAGUFULI AAHIDI KUPANDISHA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI

2


RAIS Dk John Magufuli amewataka wafanyakazi kuendelea kujenga uchumi wa nchi huku akiahidi kuwapandishia mishahara kabla kipindi chake cha urais hakijahisha.

Rais Magufuli amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa yalifanyika mjini Iringa.

Akizungumza katika Uwanja wa Samora zilimofanyika sherehe hizo, Rais Magufuli alisema; “Tunatakiwa tuujenge uchumi wetu ili tujitengenezee maisha mazuri zaidi baadae na siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu.”

Mbali na kulipa madeni, kutoa ajira mpya , kutoa elimu bure, Dk Magufuli alisema serikali yake inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya umeme, reli, viwanja vya ndege, ndege, barabara, afya, elimu na mingineyo ambayo ikamilika itakuza uchumi ambao matokeo yake ni pamoja na kulipa mishahara mizuri zaidi.

Kwa mtazamo wake alisema, serikali yake haiwezi kufanya mambo yote mawili kwa pamoja, kupandisha mishahara na kutekeleza miradi kwa kuwa yote hayo yanategemea chungu kimoja.

“Tuendelee kujenga uchumi wetu ili baadae tuwe na mishahara mizuri, tukitekeleza miradi hii yote nayosema najua hautachukua muda mrefu mishshsra itaoinngezeka na hili halitasubiri hadi mei mosi nyingine ije,” alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment