![]() |
Mwimbaji
wa muziki wa Injili ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi,
Dk Tumaini Msowoya amefanikiwa kuachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa ‘Nina
Furaha’.
Akizungumza
na wanahabari, Dk Tumaini alisema video hiyo ipo kwenye albamu yake ya ‘Hakuna
Matata’ iliyobeba nyimbo nane.
“Ni
video ya kwanza na ina nyimbo ambazo mtu akizitazama moyo wake utajaa furaha
hata kama ana huzuni,” alisema.
Alisema
wimbo wa Nina Furaha unampa mtu nguvu ya kusonga mbele na unaeleza wazi kwamba
mtu mwenye tumaini anayo furaha kwa sababu Mungu ndiye kiongozi wake.
Alisema
video hiyo ameifanya na Jmic Pro chini ya Director John Gabriel huku audio
ikiandaliwa na JB Production inayoongoza na Producer, Baraka Smart Billionaire.
“Ninachoomba
zaidi ni sapoti yenu, video itakuwa kwenye Youtube Account yangu kwa hiyo,
naomba muitazame na hiyo ni sapoti kubwa sana kwangu,” alisema.
Alitaja
nyimbo nyingine zilizo kwenye albamu hiyo ya Hakuna Matata kuwa ni Wanawake,
Mungu Mkuu, Amenitengeneza, Samehe na Mwamba.
0 comments:
Post a Comment