Tuesday, 3 April 2018

MBOWE, VIONGOZI WA CHADEMA WADHAMINIWA

Image result for viongozi wa chadema wapata dhamana


VIONGOZI sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamekamilisha masharti ya dhamana.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imejiridhisha na nyaraka walizoziwasilisha wadhamini kwa ajili ya dhamana ya washtakiwa hao na imewapa dhamana kwa maelekezo ya kuwepo mahakamani kila wanapohitajika.

Masharti ya dhamana yao ni kusaini bondi ya Sh Milioni 20, kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka ofisi za Serikali za mitaa au vijiji na kuripoti kituo kikuu cha Polisi kila Alhamisi.

Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, manaibu katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho, Ester Matiko.

Viongozi hao wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment