Tuesday, 3 April 2018

MASOGANGE AKUTWA NA HATIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Image result for MASOGANGE


MSANII wa muziki, Agnes Gerald maarufu Masogange amekutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya na kuhukumiwa kwenda jela au kulipa faini.

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, ametoa hukumu hiyo leo Aprili 3 na kuieleza mahakama kuwa Masogange katika kosa la kwanza amekutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na kosa la pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

“Hivyo katika kosa la kwanza, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh1 milioni na kwa kosa la pili, amehukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh500, 000,” amesema Hakimu Mashauri.

Februari 17 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaeleza wanahabari kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa iwapo anatumia dawa hizo za kulevya.

Awali, kabla ya kupimwa, Masogange alikamatwa na polisi akituhumiwa kutumia dawa hizo.

Masogange ni mrembo (video queen) anayetamba katika video za wasanii maarufu nchini. Mwaka 2013, alikamatwa na shehena ya kemikali bashirifu zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya, Afrika Kusini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment