Wednesday, 18 April 2018

KIKWETE KUHUDHURIA HARUSI YA ALI KIBANdoa ya mwanamuziki Alikiba na mchumba wake Amina inatarajiwa kufungwa kesho alfajiri katika msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo jijini Mombasa.

Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Asma Said anasema ndoa hiyo itafungwa katika msikiti huo uliojengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Anasema baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.

Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Ommy Dimpoz.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment