Wednesday, 4 April 2018

CHADEMA WAPOTEA BUNGENI LEO

Image result for bungeni leo


Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu leo, ni mbunge mmoja tu wa Chadema ndiye aliyeonekana ndani ya ukumbi wa Bunge katika kikao cha pili cha mkutano wa Bunge la bajeti.

Aliyeonekana katika kikao cha bunge cha leo Aprili 4 hadi saa 5:35 asubuhi, wakati Waziri Mkuu akisoma bajeti yake, ni Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga.

Awali, Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea aliingia katika kipindi cha maswali na majibu lakini akatoka baada ya kukaa kwa dakika chache.

Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, alionekana katika viwanja vya bunge asubuhi na hakuonekana tena na mbunge wa Liwale (CUF) Zuberi Kuchauka, alihudhuria kipindi cha maswali na majibu asubuhi na kuuliza swali la Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee.

Waziri Mkuu leo, anawasilisha bungeni mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge.

CHANZO; mwananchi online

Reactions:

0 comments:

Post a Comment