Sunday, 11 February 2018

MAKAMU WA RAIS AKIFAGILIA KIWANDA CHA KARATASI MUFINDI


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua ujenzi wa jengo la maabara linalojengwa na Kiwanda cha Karatasi Mufindi (MPM ) kwa kiasi cha shilingi milioni 450.

Akiwatubia wananchi wa Mgololo wilayani Mufindi mkoani Iringa Leo, makamu wa rais amepongeza jitihada za kiwanda hicho kwa kusaidia ujenzi huo na ahadi zao katika sekta ya afya na elimu.


Alisema serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na wawekezaji ikiwemo kampuni hiyo ya MPM katika kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo na kutaka wananchi kuishi vema na wawekezaji hao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment