Friday, 2 February 2018

KINGUNGE KUZIKWA MAKABURI YA KINONDONI JUMATATU

Image result for kingunge ngombale mwiru

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.

Kingunge amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa anatibiwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment