Sunday, 11 February 2018

CHADEMA YAMLALAMIKIA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO KINONDONI

Image result for uchaguzi kinondoni

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemlalamikia msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni ikidai anaashiria kuharibu uchaguzi wa Februari 17,2018 na Meneja kampeni wa Chadema Kinondoni, Saed Kubenea amesema kila linalopangwa kutaka kuuharibu uchaguzi huo hawatalikubali.

Chama hicho kimedai kutowapa viapo mawakala jana Februari 10, 2018 kunaashiria njama za kutaka wasishiriki shughuli za upigaji na kuhesabu kura.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema sheria inataka mawakala wa upigaji kura kula kiapo cha kutunza siri siku saba kabla ya kupiga kura na wanapaswa kupewa kiapo hicho.

"Anayeapisha ndiye anayesaini, hawezi kuapa mbele ya mtu mmoja na kusaini mwingine, kwa kila mwapishaji katika kila kata anakuwa na sababu zake, msimamizi wa uchaguzi anatumika," alidai Kigaila.

Kigaila amesema, "Kinachoendelea Kinondoni ni tofauti na Siha, kule Siha wameapa jana na kila wakala ameondoka na kiapo chake, sasa sijui sheria inayotumika Siha ni tofauti na inayotumika Kinondoni.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment