Thursday, 1 February 2018

ASAS MWANASIASA ANAYETABIRIWA KUKUTANA NA WENGI ZAIDI IRINGA 2018

Image result for SALIM ASAS


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Salim Abri Asas anatabiriwa kukutana na watu wengi kuliko mwanasiasa mwingine yoyote mkoani Iringa  katika kipindi cha mwaka huu 2018.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema, Asas atapata mafanikio hayo kwa kupitia kazi zake za kisiasa atakazokuwa akizifanya kama mjumbe wa NEC na kwa namna anavyoshiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kupitia nafasi yake ya NEC
Asas amekwishaanza kukutana na makundi mbalimbali ya siasa ya ndani ya CCM kupitia mialiko na shughuli za kawaida za kisiasa mjini Iringa.

Kwa kupitia mialiko hiyo Asas amekwishakutana na mabaraza ya vijana, wanawake na wazazi katika maeneo tofauti mjini Iringa lakini pia ameshiriki mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa lengo la kumpongeza diwani mteule wa kata ya Kihesa July Sawani.

Na katika shughuli za kawaida za siasa MNEC huyo amekuwa akikutana na makundi ya watu, mtu mmoja mmoja, taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo; hiyo ikitokana na michango yake mingi anayotoa kwenye miradi na shughuli za maendeleo ya watu wa Iringa.

Ameanza na anaendelea kuyafanya haya mjini Iringa na huo hautakuwa mwisho wa safari hiyo; anatarajiwa pia kukutana na makundi mengi katika wilaya zingine zote za mkoa wa Iringa kwa shughuli za kisiasa na kimaendeleo.

Mkoa wa Iringa una wilaya tatu zenye jumla ya halmashauri tano. Wilaya hizo ni Iringa yenye halmashauri ya wilaya ya Iringa na Manispaa ya Iringa, wilaya ya Mufindi yenye halmashauri ya Mji wa Mafinga na wilaya ya Mufindi na wilaya ya Kilolo yenye halmashauri moja ya Kilolo.

Katika shughuli za maendeleo
Kwa miaka mingi Asas amekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya mkoa wa Iringa.

Sekta nyingi ikiwemo ya afya, elimu, miundombinu ya barabara na maji, kilimo, biashara na michezo  zimeguswa kwa michango yake ya fedha, vifaa na mingineyo.

Kwa namna anavyojitoa kuchangia sekta hizo na zinginezo; na kwa namna anavyoshiriki katika shughuli za raha na shida kwa mtu mmoja mmoja, makundi ya watu na taasisi binafsi na zile za umma, Asas amekuwa akipokea maombi mengi na kwa namna alivyomkarimu na anavyoshughulika na maombi hayo imemfanya akutane na watu wengi.

Kwa muktadha huo, huyu ndiye mwanasiasa anayetabiriwa kukutana na watu wengi zaidi kuliko mwanasiasa mwingine mkoani Iringa.


Asas alichaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC Desemba 5, mwaka jana kwa kura 502 dhidi ya kura 74 alizopata Marcelina Mkini na 15 alizopata Benard Mbungu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment