Friday, 2 February 2018

AJALI YA NDEGE ZANZIBAR YAUA MARUBANI WAWILI


Marubani wawili wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya ndege iliyotokea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar walipokuwa wakiifanyia majaribio ya kuruka wakati wa matengenezo.

Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Tropical Air, David Kisusi amesema ndege hiyo ilianguka na kuungua jana, Alhamisi Februari Mosi saa saba mchana  na kuua marubani hao waliotajwa kuwa ni injinia Edger Alfred Mcha (26) na Dominic Bomani (64).

Kisusi amesema ndege hiyo 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ni mali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) iliyokuwa Zanzibar kwa matengenezo.


Daktari bingwa wa uchunguzi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk Msafiri Marijani amesema vifo vya marubani hao vimesababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali na kuathiriwa na moto. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment