Monday, 15 January 2018

UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA KIMARA KILUVYA WANUKIA

Related image

Ujenzi wa barabara ya njia sita kuanzia Kimara hadi Kiluvya, unatarajia kuanza mwezi ujao pindi mkandarasi atakapopatikana.

Nyumba takribani 2,000 zilizokuwa zimejengwa ndani ya mita 121.5 ya Barabara ya Morogoro zilibomolewa ili kupisha ujenzi huo ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji.

Kazi ya ubomoaji iliacha vilio kwa wakazi wa maeneo ya Kimara hadi Kiluvya huku nyumba za kifahari zikiwamo za viongozi wa Serikali na wanasiasa maarufu akiwamo Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa J na nyumba ya mke wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa iliyopo Kibanda cha Mkaa Mbezi, zikibomolewa.

Ubomoaji huo pia, ulizikumba nyumba za ibada 32, vituo vya afya vitano, vituo vya mafuta sita majengo ya Serikali manne pamoja na Shule ya Msingi Kimara ambayo ilibomolewa nusu.Reactions:

0 comments:

Post a Comment