Friday, 5 January 2018

RUGEMALILA ATAJA WEZI WA AKAUNTI YA ESCROW

Image result for rUGEMALILA

Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi leo Ijumaa ametaja wanaohusika wa wizi wa fedha katika akaunti ya Escrow.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Rugemarila ameiomba mahakama hiyo imruhusu kwenda nje ya nchi kwaajili ya uchunguzi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa miaka tisa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kueleza kuwa bado upelelezi wa kesi hiyo unaendelea hivyo anaomba Mahakama ipange tarehe nyingine.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Michaeli Ngalo ameuomba upande wa mastaka kuharakisha upelelezi na kama umeshindwa basi waitoe kesi hiyo itakayotajwa tena Januari 19, mwaka huu.

Baada ya wakili wake kueleza hayo Rugemarila alinyoosha mkono akimweleza Hakimu kuwa anasumbuliwa na kansa kwa muda wa miaka tisa hivyo anaomba akapatiwe matibabu India kwani uvimbe umejitokeza.

"Nilikuwa sijui kama nina uvimbe sehemu za siri, huu mwaka mpya umenijia vibaya, naomba nipewe ruhusa kwenda India kwa daktari wangu ili nikafanyiwe uchunguzi," Rugemarila alidai alishawasilisha nyaraka za ushahidi Takukuru zikionyesha nani mwizi aliyeisababishia Serikali hasara.

 "Mwizi ni Benki ya Standard Chartered iliyoko hapa nchini Tanzania Ltd na ile iliyoko Hong Kong ambazo ndio zimesababisha hasara ya Trillion 37 kwa Serikali,”

"Pia kuna nyaraka nilizozipelekaTakukuru zikionyesha wengine walioshiriki katika wizi wa fedha hizo, naomba niendelee kuwa hai ili niweze kutoa ushahidi mzuri kuhusu wezi wa fedha hizo.”

Mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ameieleza Mahakama kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano ikiwemo nyaraka zitakazoitajika.

Hata hivyo, wakili Swai alieleza Mahakama kuwa zipo nyaraka ambazo Rugemarila aliwasilisha ofisini na zinafanyiwa kazi kisha watatoa majibu baada ya kukamilika.


Hakimu Simba alisema afya za washtakiwa ni muhimu wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi na kuutaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment