Thursday, 18 January 2018

RC MASENZA AWAPA MTIHANI WAKUU WA SHULE MICHANGO MASHULENI
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amekutana na walimu wakuu kutoka wilaya zote za mkoa huo na kuwataka kuandika kwake barua ya mkono wakieleza kama kuna michango katika shule zao.

“Katika barua hizo nataka kila mmoja aeleze  kama katika shule yake kuna aina yoyote ya mchango uliopigwa marufuku, sababu za kuwepo kwake, aliyehidhinisha, kiasi cha mchango na unatolewa kwa ajili ya kazi gani,” alisema leo wakati akizungumza na walimu wa wilaya ya Iringa na Kilolo kabla hajaelekea wilayani Mufindi kwa lengo hilo hilo.

Amechukua uamuzi huo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Dk John Magufuli kuzuia aina yoyote ya michango kwa wanafunzi mashuleni.


Masenza alitoa onyo kwa walimu watakaotoa taarifa za uongo akisema hatua kali ikiwemo ya kuvuliwa wadhifa wake, zitachukuliwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment