Monday, 15 January 2018

RAIS WA LIBERIA AMALIZA MUDA WAKE KWA KUFUKUZWA KWENYE CHAMA

Image result for Ellen Johnson Sirleaf

Rais anayemaliza muda wake Ellen Johnson Sirleaf amefukuzwa kwenye chama tawala cha Unity Party (UP) ambacho kilimwingiza madarakani na kumwezesha kuongoza kwa miaka 12.

Mbali ya mwanamama huyo mshindi wa Tuzo ya Nobel, viongozi wengine watatu wametupiwa virago kwenye chama hicho ambao ni Seneta wa Kaunti ya River Gee, Commany B. Wesseh; Mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji, Madam Medina Wesseh; na Naibu katibu mkuu Patrick T. Worzie.

Taarifa ya UP iliyotiwa saini na Naibu katibu mkuu wa mawasiliano Mohammed Ali na kusambazwa kwenye vyombo vya habari Jumapili, hatua ya kufukuza rais huyo imetokana na ukiukwaji wa katiba na “vitendo vingine vya kudhuru kuendelea kuwepo na heshima ya chama.”

“Mwenendo wa watu hao waliofukuzwa … ulichangia kukihujumu na kuathiri uwepo wa chama siku zijazo,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilinukuu Ibara ya VII ya chama inayofafanua wajibu, haki na mamlaka ya wajumbe wa UP ambayo inadaiwa yalivurugwa na Rais.

“Sehemu ya 1(e) inaelezea jukumu la wanachama kwenye uchaguzi; (e) kumuunga mkono mgombea wa Unity Party kipindi chote cha uchaguzi na kumpatia msaada mwingine wowote ulio katika uwezo kwa ajili ya mgombea yeyote wa Unity Party katika uchaguzi wowote; na (f) kuwa na mwenendo ambao utakipatia heshima chama katika uchaguzi wowote;” ilisema taarifa hiyo kuhusu katiba.


Katika uchaguzi uliopita, mwanasoka nyota wa zamani duniani George Weah alimshinda mgombea wa UP, makamu wa rais Joseph Boakai. Weah ataapishwa Januari 22.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment