Sunday, 28 January 2018

MNEC ASAS KUICHANGIA UWT IRINGA VIJIJINI SH MILIONI 25MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Salim Abri Asas ameendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa mkoa wa Iringa na chama chake cha CCM, safari hii akiahidi kuuchangia Umoja wa Wanawake wa CCM Iringa Vijijini (UWT Iringa Vijijini) Sh Milioni 5 kila mwaka, kuanzia mwaka huu..

Kwa ahadi hiyo, umoja huo utapata jumla ya Sh Milioni 25 katika kipindi cha miaka mitano  ya ujumbe wake wa NEC.

“Mimi ni binadamu na katika hili nitaandika wosia, kama nitakufa kabla ya miaka mitano, nitaiambia familia yangu msiisahau ahadi niliyotoa kwa UWT Iringa Vijijini.,” alisema kwenye baraza la umoja huo lililofanyika jana mjini Iringa.

Pamoja na ahadi hiyo, Asas amesema atangaalia namna ya kuchangia ujenzi wa jengo la kulea watoto unaotarajiwa kufanya na umoja huo.

“Hili siwezi kulisema sana kwasababu uongozi mpo na sijajua mikakati yenu, sijajua michoro yenu, tutakaa na mwenyekiti tuone tunaliwekaje ili mjiongezee mapato kama sio kuwasaidia msingi basi hata mabati. Ni vizuri tuone michoro inasemaje, tukiwapatia nyavu mtajitegemea,” alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment