Tuesday, 23 January 2018

MKUU WA WILAYA AINGIA MATATANI KWA KUPIGA KAMPENI

Image result for Onesmo Buswelu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu hakufanya jambo sahihi kupanda jukwaani na kumnadi mgombea wa CCM katika Jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema ili Buswelu aweze kuchukuliwa hatua, wenye jukumu la kumshtaki ni vyama vinavyopinga jambo alilolifanya.


Alisema vyama hivyo vinatakiwa kumshtaki katika kamati ya maadili inayoundwa na wajumbe wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi katika jimbo husika na kwamba jambo hilo linapaswa kufanyika ndani ya saa 72, tangu apande jukwaani. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment