Sunday, 21 January 2018

MAJALIWA AAGIZA WAKALA WA MAJENGO MARA AKAMATWE

Image result for kassim majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Mara kumkamata na kumuhoji meneja wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wa mkoa wa Mara, mhandisi Peter Salim.

Amesema mhandisi huyo anakamatwa kutokana na kushindwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 21, 2018 na Ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa Serikali ilitoa Sh600 milioni, Aprili, 2017 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo, lakini hadi sasa wakala huo hajafanya kazi yoyote.Reactions:

0 comments:

Post a Comment