Friday, 5 January 2018

LISSU ATOKA HOSPITALI NAIROBI, AZUNGUMZIA ALIVYONUSURIKA KIFO


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kilichotokea kwake kwa maoni yake ilikuwa ni jaribio la mauaji ya kisiasa.

Amesema hayo leo Ijumaa akiwa anatoka hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

“Mimi siyo mfanyabiashara niwe nimemrusha mtu na huwa sipigani baa,” amesema Lissu.

 Amesema kuwa risasi 16 zilimpiga mwili wake, risasi nane zikatolewa Dodoma na risasi saba jijini Nairobi huku akibakiwa na moja mwilini mwake.

Ameeleza kuwa sehemu alipopigiwa risasi ni nyumbani kwake alipopangiwa na Bunge kwa kuwa yeye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni hivyo eneo ambalo anakaa ni sehemu palipo salama lakini alimiminiwa risasi 16 na waliofanya hivyo hawajulikani walipo.


Amesema kwa watu waliohesabu risasi zilizopiga gari yale ziko 38 lakini 16 ndizo zilizompata mwilini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment