Thursday, 25 January 2018

KIGWANGALLA ALIPA JESHI LA POLISI SIKU SABA

Image result for kigwangalla

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na matukio ya ujangili la sivyo atakwenda kushtaki kwa amiri jeshi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Dk Kigwangala amesema polisi wana taarifa zote kuhusiana na watu hao kuhusika katika ujangili pamoja na kula njama ya mauaji ya raia wa kigeni lakini polisi wamekuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua.


Aidha, Dk Kigwangalla ametoa siku saba kwa wakurugenzi wa makampuni ya uwindaji na ofisa mmoja wa Tanapa kufika katika kikosi maalum atakachokiunda; kwa ajili ya mahojiano kuhusu tuhuma mbalimbali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment