Thursday, 25 January 2018

DK MAGUFULI AMWALIKA RAIS WA ZIMBABWE

Image result for Emmerson Mnangagwa

Rais John Magufuli amemkaribisha Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe kutembelea nchini.

Dk Magufuli ametoa mwaliko huo leo Alhamisi Januari 25,2018 alipoagana na Balozi wa Zimbabwe nchini Edzai Chimonyo anayemaliza muda wake.


 “Naomba umwambie Rais Mnangagwa kuwa namkaribisha atembelee Tanzania na namtakia heri katika majukumu yake, natarajia ataendeleza uhusiano na ushirikiano wetu ili tuweze kujiimarisha zaidi kiuchumi kwa manufaa ya nchi hizi mbili,” amesema Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment