Wednesday, 24 January 2018

CHADEMA, CCM KUZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE KINONDONI JUMAMOSI

Image result for salum mwalimu mtulia

MACHO na masikio ya wengi yataelekezwa katika viwanja vya Jimbo la Kinondoni siku ya Jumamosi wakati vyama vya CCM na Chadema vitakapokuwa vikizindua kampeni zake za uchaguzi mdogo wa ubunge ambao kinyang’anyiro chake kinatarajiwa kuwa na mchuano mkali.

Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CUF, Maulid Mtulia kujivua uanachama wa chama hicho akisema anamuunga mkono Rais John Magufuli na baadaye alijiunga na CCM.

Mtulia amepitishwa na CCM kuwania tena ubunge jimboni humo na atachuana na Salum Mwalimu wa Chadema ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar.


Wakati CCM ikisema itazindua kampeni katika viwanja vya Biafra; Chadema haijaweka wazi eneo la uzinduzi. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment