Friday, 12 January 2018

BAADA YA LOWASSA, RUNGWE NAYE ATAKA KUKUTANA NA RAIS MAGUFULI

Image result for rungwe hashim

Mwenyekiti Chama cha Chaumma, Hashim Rungwe amesema anatamani kwenda Ikulu kuonana na Rais John Magufuli ili kumweleza mambo ambayo yatawezesha kusaidia kuleta mabadiliko katika utawala wake.

Rungwe amesema kila mtu anatamani kuonana na Rais Magufuli lakini nafasi hiyo imekuwa haipatikani.

Rungwe anatoa kauli hiyo leo ikiwa imepita siku tatu tangu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipofanya ziara Ikulu na kuzungumza na Rais Magufuli.

“Hata mimi nataka kuonana na Rais, nimekuwa natamani sana lakini hatupati nafasi hiyo, nikikutana naye tutazungumza mambo mengi, ambayo yatamsaidia yeye mwenyewe katika uongozi wake,” amesema Rungwe na kuongeza; “Sisi upinzani tulikuwa tunasema hatutaki mafisadi, hatutaki wabidhirifu au tunapiga kelele dawa hakuna hospitalini kwa hiyo anapopeleka dawa hospitalini ni sisi tumesaidia, kwa hiyo kuongoza ni kusikiliza watu wanasema nini wakati mwingine.”

Chanzo; Mwananchi

Reactions:

0 comments:

Post a Comment