Tuesday, 19 December 2017

VIGOGO WA HALMASHAURI WAPANDISHWA KIZIMBANI


Image result for takukuru

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafikisha kortini vigogo watatu wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Vigogo hao wamefikishwa mahakamani leo Jumanne Desemba 19, 2017 mbele ya Hakimu Mkazi, Arnold Kirekiano.

Mbali na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Melkzedeck Humbe ambaye sasa yuko Halmashauri ya Bariadi, wengine waliofikishwa mahakamani ni aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri hiyo Thadeus Meela na ofisa mwandamizi, Valentina Mollel.

Mwendesha mashtaka wa Takukuru, Susan Kimaro amedai Julai 8,2014 washtakiwa walighushi nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri na kufanya malipo ya Sh27 milioni.


Washtakiwa wamekana mashitaka na wameachiwa kwa dhamana. Wamedhaminiwa kwa bondi ya Sh5 milioni kila mmoja na kesi imepangwa kutajwa Februari 15, mwakani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment