Friday, 15 December 2017

SAMIA AHAMIA RASMI DODOMA LEO


Makamu wa Rais, Samia Suluhu leo Ijumaa Desemba 15 amehamia rasmi makao makuu ya nchi ikiwa ni mwendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo.

 "Nilikuwa hapa kwa muda mrefu kidogo lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba 15 na nimefurahi kwamba nitafanya kazi mahala pangu pa kazi pa kudumu," amesema Samia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment