Saturday, 2 December 2017

ODINGA NAYE KULA KIAPO DESEMBA 12

Image result for Odinga

Katika hali ya kushangaza, Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameanza kutoa na kusambaza kadi za mualiko kwa ajili ya hafla ya kuapishwa kwake kama Rais wa Watu wa Kenya.

Kadi ya mualiko huo inaonyesha shughuli hiyo itafanyika Desemba 12, mwaka huu ikiwa ni siku chache tu tangu Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kula kiapo cha awamu ya pili ya uongozi wake mbele ya maelfu ya Wakenya na Viongozi wa Mataifa mbalimbali wapatao 60 katika Uwanja wa Kasarani.

Odinga, amekuwa akisisitiza kuwa Kenyatta sio Rais wa chaguo la watu bali amepandikizwa kwa nguvu ya mfumo ‘system’, na kwamba yeye ndiye chaguo la watu.


Aidha, amesema kuwa kuapishwa kwake hakutakuwa kwa usanii na mzaha kama ilivyotokea kwa kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kiiza Besigye na kudai kuwa eneo na muda utakaofanyika tukio hilo vitatangazwa hapo baadae.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment