Saturday, 9 December 2017

MWENYEKITI RUVUMA PRESS CLUB AJITOSA UBUNGE SONGEA MJINI

Image result for kuchonjoma

MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Songea, Andrew Kuchonjoma ni mmoja kati ya wanachama 13 wa CCM waliochukua fomu za kugombea  ubunge Jimbo la Songea Mjini kuziba pengo baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Leonidas Gama.

Kuchonjoma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) atalazimika kuachia ngazi nafasi zote katika sekta hiyo ya habari endapo jina lake litapitishwa na vikao vya chama hicho kuwania nafasi hiyo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Songea mjini, Juma Mpeli amesema wanachama hao wamechukua fomu na wanatarajia wanachama wengi zaidi kujitokeza.

Wengine waliochukua fomu ni John Nchimbi, Gideon Ole Lairumbe, Mussa Ndomba na Kayoya Fuko.

Yupo pia Mwanasheria Dk Damas Ndumbaro, Francis Miti, Imman Lipuka na Dk Theresa Uvisa.

Amewataja wanachama wengine ni Prosper Luambano, Shaweji Mfaume, Getrude Haule pamoja na Raymond Mhenga ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma.


Amewataka wanachama wa CCM Jimbo la Songea mjini kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwani mwisho wa kuchukua fomu ni leo Desemba 9 saa 10 jioni.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment