Wednesday, 6 December 2017

KUBENEA AZUNGUMZIA THAMANI YAKE AKIKANUSHA KUHAMA CHADEMA

Image result for kubenea

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amekanusha taarifa zilizosambaa hivi karibuni zikimhusisha kutaka kuhama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kubenea amesema hayo leo mbele ya wanahabari na kudai kuwa hajawahi kuongea na chombo chochote cha habari wala mtu wa CCM.

Amesisitiza kuwa hana mpango wa kukihama chama chake kama inavyosambazwa mitandaoni.

“Sijawahi kuhongwa, mimi sina bei, bei yangu ni utu wangu. Hizi zote ni propaganda za CCM ili wasihojiwe mambo ya msingi, wamesema wanatoa milioni 50 kila kijiji ziko wapi. Mimi sina mpango wowote wa kuondoka Chadema na sijawahi kuzungumza na mtu yeyote kuhama Chadema,” amesema Kubenea.

Amesema CCM inarudisha biashara ya utumwa ya kununua watu na kwamba Mbunge wa Arumeru Mashariki alipeleka ushahidi TAKUKURU, lakini tunaona Rais alimpandisha cheo mtuhumiwa, hivyo hawezi kujiunga na chama hicho hata siku moja.


 “Sinunuliki hata kwa Bajeti nzima ya serikali,” amesisitiza Kubenea. Kubenea ni miongoni mwa wabunge 9 kutoka UKAWA waliodaiwa kuwa wapo njiani kuhamia CCM ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Kibamba (Chadema), Mhe. John Mnyika

Reactions:

0 comments:

Post a Comment