Friday, 8 December 2017

DED WA NKASI ATUMBULIWA, NI JULIUS KAONDO

Image result for Mkurugenzi wa Nkasi Julius Kawondo

Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh Bilioni 7.

Jafo amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

"Natumia Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na Sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," amesema Jafo.


Jafo amemuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika Kijiji cha Kamwanda wilayani humo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment