Monday, 4 December 2017

CCM MKOA WA IRINGA KUPATA VIONGOZI WAKE KESHOMACHO na masikio ya wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, kesho yataelekezwa katika ukumbi wa Kichangani mjini Iringa kutakakofanyika uchaguzi mkuu utakaochagua viongozi wakuu wa chama hicho watakaokiongoza kwa miaka mitano ijayo.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya chama hicho kupata viongozi wake wote katika ngazi ya wilaya na jumuiya za chama hicho, UWT, UVCCM na Wazazi ngazi ya wilaya na mkoa.

Katika nafasi nyeti ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Salim Asas anawania nafasi hiyo pamoja na Marcelina Mkini na Bernard Elias Mbungu.

Wabashiri wa mambo ya siasa wanatoa nafasi kubwa kwa Salim Asas kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti, mchuano mkali unabashiriwa kuwa kati ya Mkuu wa Wilaya Mstaafu Evans Balama na kada kijana wa chama hicho Albert Chalamila. Mwingine anayewania nafasi hiyo ni Daniel Kidava.


Katika uchaguzi huo, chama hicho pia kitawapigia kura Mwinyiheri Baraza, Andrew Ghemela na Josia Kifunge wanaowania nafasi moja ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment