Monday, 27 November 2017

SERIKALI KUSAMBAZA KONDOMU ZA BURE MILIONI 500

Image result for salama kondomu

Serikali inatarajia kununua na kusambaza bure kondomu zaidi ya milioni 500 nchi nzima kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamaila, amesema kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund.

Amesema mipira hiyo ya kiume itasambazwa kupitia mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya baa, nyumba za kulala wageni, migodini na katika kumbi za burudani katika mkakati wa kitaifa wa kusambaza kondomu.


“Takwimu za mwaka 2011/12 zinaonyesha asilimia 69 ya wanawake na asilimia 77 ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU lakini ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,” amesema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment