Sunday, 12 November 2017

NYALANDU ASHINDWA KUHUTUBIA MKUTANO WA CHADEMA MTWARA

Image result for nyalandu

Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyejiondoa CCM siku 12 zilizopita ameshindwa kupanda jukwaani mjini Mtwara katika mkutano wa Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana Jumamosi Novemba 11,2017 akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam alisema amempokea Nyalandu na leo Jumapili Novemba 12,2017 angeungana naye kwenye mkutano wa kampeni mjini Mtwara.


Kukosekana kwa ndege inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mtwara kumemsababishia Nyalandu kushindwa kuhudhuria mkutano huo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment