Tuesday, 7 November 2017

NAPE ATAKA CCM IAMBIWE UKWELI

Image result for Nape nnauye

Nape Nnauye ameonya kuwa endapo chama hicho hakitataka kuambiwa ukweli na kukosolewa, utakuwa mwanzo wa kuanguka kwake.

Nape aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, amesema endapo CCM itaua utamaduni wa kukosoana kupitia vikao itapoteza mwelekeo.

“Hiki chama tukifika mahali tukaanza kufanyiana unafiki kwamba hatutaki kuambiana ukweli tunapokosea utakuwa ndiyo mwanzo wa kuanguka kwa CCM.” Amesema hayo juzi nyumbani kwake eneo la Kisasa mjini Dodoma katika mazungumzo maalumu na gazeti la Mwananchi.

Nape ambaye leo anatimiza miaka 40 ya kuzaliwa, ameeleza kusikitishwa na namna ya baadhi ya watu aliowaita “vijana wa CCM”, kupotosha kwa makusudi kauli na ujumbe wake anaoutuma kupitia mitandao ya Twitter na Instagram.

“Kuna ambao wanamchukia tu Nape kwa sababu wanadhani alishiriki kuzuia wagombea wao na hasa hawa vijana wafuasi wa Edward Lowassa ambao bahati mbaya alipohama hawakuhama naye,” alisema.

“Hawa nao wako wanapitia humo kusema hasira zao. Mara Nape huyu anamsema Rais. Unamuona Nape huyu anaisema Serikali. Hawa nao tuwapuuze. Wakikua wataacha.


“Wanaona Nape ni beki mzuri wa kufanyia mazoezi au ya kuonekana wapo ili tu wapewe vyeo. Bahati nzuri mimi nimekulia ndani ya CCM najua lipi zuri na lipi baya kwa CCM,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment