Monday, 27 November 2017

MZALENDO MILIONEA WA IRINGA APANDISHWA KIZIMBANI
MFANYABIASHARA maarufu wa mjini Iringa, Rodrick Allon maarufu kwa jina la Mzalendo na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa wakituhumia kutumia vibaya mashine za kielektroniki za kodi (EFD) na kushindwa kurejesha kodi serikalini.

Wengine katika kesi hiyo Namba 23 ya mwaka 2017 iliyotajwa kwa mara ya kwanza leo katika mahakama hiyo ni pamoja na Exaud John na Oswald Njole ambao ni wasaidizi wa mfanyabishara huyo.


Watuhumiwa wako nje bila masharti yoyote mpaka kesho mahakama hiyo itakapojadili suala la dhamana yao.

Kabla ya kuachiwa huru, watuhumiwa hao walikwa kwa muda katika mahabusu ya mahakama hiyo.

Mzalendo ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa mjini Iringa anayejishughulisha na biashara ya vifaa vya ujenzi, nyumba za kulala wageni, usafirishaji na usambazaji wa vinywaji mbalimbali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment