Wednesday, 15 November 2017

MUGABE MAJI YA SHINGO

Image result for MUGABE

Aliyekuwa Makamu wa Rais, Emerson Mnangagwa leo ametangazwa kuwa Rais mpya wa Chama cha ZANU-PF na kutua Uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Manyame akitokea uhamishoni.

Mnangagwa alikimbilia uhamishoni hivi karibuni baada ya kufutwa kazi ya Umakamu wa Rais na Rais, Robert Mugabe.

Aidha, Jeshi hilo la Zimbabwe linawashikilia Waziri wa Fedha, Ignatius Chombo, Waziri wa Elimu, Prof. Jonathan Moyo na Afisa Mwandamizi ndani ya chama cha ZANU-PF Savior Kasukuwere.


Wakati huohuo, taarifa kutoka vyanzo vya ngazi za juu zinadai kuwa Rais Robert Mugabe mwenye miaka 93, anajiandaa kujiuzulu kufuati usiku uliotawaliwa na milio ya risasi na makazi yake kuzingirwa na Jeshi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment