Friday, 17 November 2017

MUGABE AONEKANA HADHARANI

Mr Mugabe surrounded by people including one man in full uniform

Rais Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi lilipomweka chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya leo kuhudhuria mahafali ya chuo kikuu.

Akiwa amevalia joho la kisomi lenye rangi za bluu na njano na kofia, Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikaa kwenye kiti mbele kabisa kwenye ukumbi na alishangiliwa kwa mbinja na vigelegele alipotangaza kwamba mahafali yamefunguliwa.


Mkongwe huyo aliyetawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, kwanza akiwa waziri mkuu (1980 hadi 1987) na baadaye rais (1987 hadi sasa) aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwake kuanzia Jumanne ikiwa ni wiki moja baada ya kumfuta kazi aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment