Monday, 13 November 2017

MSANII LULU ATUPWA JELA MIAKA MIWILI

Image result for elizabeth Lulu mahakamani leo

Mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo imetolewa muda mfupi uliopita, leo Jumatatu, katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba.

Watu mbalimbali wamejitokeza kufuatilia hukumu hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Maelezo ya Jaji Rumanyika: Ushahidi umejikita kwenye ushahidi wa mazingira hata mtuhumiwa alikubali.


Mtuhumiwa alikubali marehemu alikuwa mpenzi wake na alikuwa naye siku ya tukio.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment