Tuesday, 14 November 2017

MPANGO WA KUIFUTA TTCL WAIVA

Image result for ttcl

Serikali iliwasilisha Muswada wa Sheria ambao unaiua rasmi Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kuanzisha shirika jipya la mawasiliano Tanzania ambalo litamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

Muswada huo, umewasilishwa bungeni leo Jumanne na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa huku wabunge wakipinga baadhi ya vifungu vya muswada huo.

Akiwasilisha muswada huo, Profesa Mbarawa amesema madhumuni yake ni kuanzisha shirika hilo kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma kwa jamii.

Profesa Mbarawa amesema sheria hiyo mpya itaiwezesha TTCL kutekeleza majukumu yake kama shirika la umma la mawasiliano likijulikana kama Tanzania Telecommunication Corporation.

Amesema mambo muhimu ya kuzingatiwa katika muswada huo ni kuwa unakwenda kuifuta TTCL na kuanzisha shirika jipya.


Sheria hiyo ambayo itaumika Tanzania bara na Zanzibar, ilipendekeza muundo wake na mtendaji mkuu na wajumbe watano ambapo upande wa Tanzania Zanzibar utakuwa na mjumbe mmoja.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment