Friday, 10 November 2017

MGOMBEA WA CHADEMA KITWIRU KUBORESHA ELIMU YA SEKONDARI


MGOMBEA udiwani wa kata ya Kitwiru, Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bahati Chengula ameahidi kusimamia na kukamilisha mchakato wa ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondati Ipogolo endapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo.

Katika mkutano wake wa kampeni alioufanya jana katika mtaa wa Kaloleni, Chengula amesema katika kipindi atakachokuwa madarakani kama diwani wa kata hiyo moja ya ajenda yake kuu ni kuboresha sekta ya elimu katika kata hiyo na kwa kuanzia atahakikisha shule hiyo ya sekondari inapata kidato cha tano na sita.

“Nitaifanya kazi hii kwa nguvu zangu zote nikishirikiana na nguvu za wananchi wangu kuhakikisha shule yetu ya sekondari inakuwa ya viwango vya juu na taasisi zingine zote za elimu katika kata hii zinatoa huduma katika mazingira bora,” alisema.

Alisema watu wa Kata ya Kitwiru ni watu wenye hali ya kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo lakini wamekuwa wakikatishwa tama na watu wachache wanaokusanya michango hiyo na kuitumia kwa faida zao.

“Nitahakikisha kunakuwepo na uwazi wa hali ya juu kwa kila jambo linalofanywa katika kata yetu ili wananchi wawe sehemu ya maendeleo tunayoyatafuta,” alisema huku akisisitiza kwamba hakuna serikali inayoweza kutekeleza mipango yake yote ya maendeleo bila kushirikisha nguvu za wananchi.

Ombi langu kwenye ifikapo Novemba 26 amkeni mapema, wahi katika kituo chako cha kupigia kura na piga kura ya dhahabu itakayompa ushindi mkubwa Bahati Chengula ili awe diwani wako, alisema.


Alisema kumchagua Bahari Chengula ni kutoiyumbisha kata kisiasa na kimaendeleo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment