Tuesday, 21 November 2017

MCHUNGAJI MSIGWA AWAPIGIA MAGOTI WANA CCM WA KITWIRU

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mchungaji Peter Msigwa amewaomba wana CCM wa kata ya Kitwiru kumnyima kura mgombea wa chama hicho akikumbushia jinsi alivyowatukana na kuwadharau wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Katika uchaguzi huo, CCM imemsimamisha Baraka Kimata aliyekuwa diwani wa kata hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kabla hajatimkia CCM.


“Wana CCM mmedharauliwa sana , onyesheni nyinyi ni wa thaman, kwanini mletewe mtu aliyewatukana mwaka 2015 mpaka akashinda uchaguzi huo, hiyo ni dharau kubwa kwenu,” alisema katika mkutano wa kumnadi mgombea wa kata hiyo kupitia Chadema, Bahati Chengula.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment