Wednesday, 15 November 2017

MBOWE KUTUA IRINGA MJINI KESHO, WEMA NAYE KUANDALIWA MKUTANO

Image result for mbowe wema

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kesho atakuwa mjini kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata Kitwiru.

Katika uchaguzi huo, Chadema wamemsimamisha Bahati Chengula anayewania nafasi hiyo ya uwakilishi dhidi ya vyama vingine vya siasa, kikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM).

CCM ambao ni washindani wakuu wa Chadema katika uchaguzi huo wamemsimamisha Baraka Kimata aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka miwili iliyopita kupitia Chadema kabla hajajieungua na kujiunga na CCM waliomsimamisha tena kuwania nafasi hiyo baada ya kushinda kura za maoni za cahama hicho.

Wakati Mbowe akitarajia kutua mjini Iringa kesho, chama hicho kiko katika mipango ya kumleta msanii maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu ili naye aje atete na wadada wenzake wa kata hiyo.


Mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema mawasiliano na mlimbwende huyo aliyejiunga na chama hicho hivikaribuni yanaendelea kupitia viongozi wengine wa chama.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment