Saturday, 11 November 2017

MAFINGA MJI YAANZA KUBORESHA KITUO CHA AFYA CHA IHONGOLE

Image result for cosato chumi

Halmashauri ya Mji wa Mafinga imeanza kuboresha kituo chake cha afya cha Ihongole, mpango utakaogharimu zaidi ya Sh Milioni 500 zilizotolewa na serikali.

Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi amesema maboresho hayo yanahusisha ujenzi wa maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, kichomea taka, na nyumba ya daktari.

Alisema kituo hicho cha afya kinaboreshwa ikiwa ni utekelezaji wa moja kati ya ahadi zake za kuboresha sekta ya afya katika jimbo hilo aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi wa 2015.

“Yote haya yanawezakana kwasababu ya ushirikiano mkubwa baina yangu kama mbunge, mkuu wa wilaya, waheshimiwa madiwani, mkurugenzi wa halmashauri na watendaji wake, serikali na wananchi,” alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment