Friday, 10 November 2017

KIMATA AZUNGUMZIA ANGUKO LA CHADEMA, UKAWA

MGOMBEA udiwani wa kata ya Kitwiru, Iringa Mjini kwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Baraka Kimata amekifananisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na gari lisilo na matairi lenye madereva wanaoamini linaweza kufika mwisho wa safari likiwa katika hali hiyo.

Ametoa ujumbe huo mzito kwa wakazi wa mtaa wa Mnazi Mmoja jana wakati akiwaomba wamchague kuwa diwani wao katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika Novemba 26.

Kimata anagombea udiwani wa kata hiyo ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuachia wadhifa huo aliokuwa wakiushikiria kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alichosema hakina muelekeo kwasababu gari lake halina tena matairi.

Kimata alisema miaka miwili iliyopita Chadema iliingia katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 ikiongoza umoja wa vyama zaidi ya vitano vilivyojinadi kuing’oa kupitia Ukawa lakini leo wamesambaratika vibaya, matairi ya gari waliyokuwa wakitumia yamepasuka, halafu wanajitapa kufika mwisho wa safari.

“Katika uchaguzi huu mdogo, Chadema wanamgombea wao, CUF wana mgombea wao na NCCR-Mageuzi wana mgombea wao, angalieni tairi za gari yao wanavyozipasua, watafikeje safari wanayoitaka,” alisema.

Aliwaomba wapiga kura wa kata hiyo kumchagua tena kuwa Diwani wao, safari hii akipitia CCM aliyoifananisha na gari lenye tairi imara, lenye uhakika wa safari yake na linalosimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia ngazi ya mtaa hadi Ikulu.


Mgombea huyo na chama chake hicho, leo wanaendelea na kampeni zao katika mtaa wa kisiwani darajani

Reactions:

0 comments:

Post a Comment