Saturday, 25 November 2017

KESHO NDIO KESHO, NI AMA CHADEMA AU CCM UCHAGUZI KATA YA KITWIRU
MACHO na masikio ya wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini kesho yataelekezwa katika kata ya Kitwiru kunakofanyika uchaguzi mdogo wa udiwani unaoshirikisha vyama zaidi ya viwili huku Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vikipewa nafasi kubwa ya kushinda.

Wakati Chadema wametabiri mgombea wao kushinda kwa asilimia zaidi ya 70 katika kata hiyo, CCM kwa upande wao wanasema hakuna shaka kwamba mgomea wao ataibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho.


Wagombea hao ni Bahati Chengula wa Chadema na Baraka Kimata wa CCM.

Kampeni za uchaguzi huo zinafungwa leo huku CCM ikimualika kwa mara nyingine tena Mbunge wa Mtera na Mjumbe wa NEC CCM, Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji, Chadema wao watakuwa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment