Tuesday, 14 November 2017

HAT TRICK YAMPA MPIRA MSHAMBUALIAJI WA MAPOGOLO FC


MCHEZAJI wa Mapogolo FC , Emmanuel Sade amekabidhiwa mpira wake baada ya kufunga hat trick katika mchezo war obo fainali ya kwanza ya Kombe la SPANEST Piga Vita Ujangili, Okoa Tembo dhidi ya Mahuninga FC.


Ligi hiyo inayofanyika kwa mwaka wa nne sasa ilianzishwa na Spanest ambao ni Mradi wa Kuboresha Mtandano wa Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania ikilenga kuwahamasisha wananchi wa vijiji 24 vya tarafa za Idodi na Pawaga zinazopakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa upande wa wilaya ya Iringa kushiriki katika vita dhidi ya ujangili na kuokoa maisha ya Tembo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment