Tuesday, 21 November 2017

DK MWAKYEMBE KUZINDUA MICHUANO YA SHIMUTA MJINI IRINGA KESJO

Image result for mwakyembe

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kesho Jumatano atamwakilisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa michuano ya SHIMUTA inayofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Samora, mjini Iringa.

Michuano hiyo inayohusisha wafanyakazi wa mashirika ya umma, kampuni za watu binafsi na taasisi mbalimbali zilizopo nchini ilianza Novemba 19 na itahitimishwa Desemba 1.

Akizungumza na wanahabari mjini Iringa jana, Mwenyekiti wa SHIMUTA, Dk Hamis Mkanachi alisema michuano hiyo inashirika timu mbalimali kutoka taasisi mbalimbali 23.

“Mahudhui ya mwaka huu ni kuunga mkono juhudi za serikal katika kuhamasisha uchumi wa viwanda sambamba na kuinua na kuendeleza michezo mahali pa kazi,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa SHIMUTA, Chacha Maginga alitaja michezo inayochezwa kuwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, riadhaa, mpira wa meza, na mchezo wa vishale.

Maginga alisema mbali na serikali michuano hiyo inafadhiliwa na kampuni ya Maji Mkwawa, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kampuni ya pipi Ivory na kampuni ya maziwa ya Asas.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment