Thursday, 9 November 2017

CHADEMA YAMNADI MGOMBEA WAKE KITWIRU IKISEMA HANA NJAACHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemnadi mgombea wake udiwani kata ya Kitwiru Iringa Mjini kikisema hana njaa, anawania nafasi hiyo kwa lengo moja tu la kuwatumikia wananchi wa kata hiyo.

Chadema imemsimamisha Bahati Chengula katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 26, mwaka huu.

“Huyu ni mgombea mwenye dhamira ya dhati ya kuwapigania wananchi wa kata hii, hajaja kutafuta fedha,” alisema Kamanda Mbuma wakati akimpigia debe katika mtaa wa Uyole B.

Aidha chama hicho kimesema hakisombi watu kwa ajili ya kwenda kwenye mikutano yake inayoendelea katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo kwakuwa kinataka ujumbe wake ufike kwa wapiga kura halisi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment