Sunday, 26 November 2017

CHADEMA TAABANI CHAGUZI NDOGO ZA UDIWANI KITWIRU NA KIMALA


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimekigalagaza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika chaguzi ndogo mbili za udiwani zilizofanyika mkoani Iringa hii leo.

Chaguzi hizo zilifanyika katika kata ya Kitwiru  mjini Iringa na Kata ya Kimala wilayani Kilolo sambamba na kata zingine 41 katika maeneo mbalimbali nchini.

Wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea taarifa za awali zinaonesha CCM ilikuwa ikiongoza kwa tofauti ya kura nyingi katika vituo vingi vya kata hizo.

Matokeo yaliyotufikia hivi punde yanaonesha mgombea wa CCM katika kata ya Kimala, Amoni Kikoti ameshinda uchaguzi huo kwa kuzoa kura  1,104 dhidi ya kura 718 alizopata mgombea wa Chadema Tumson Kisoma.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment