Monday, 13 November 2017

CCM, CHADEMA WACHUANA IDADI YA WAFUASI UCHAGUZI MDOGO KITWIRUIDADI ya wananchi wa kata ya Kitwiru wanajitokeza katika mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru mjini Iringa inaoonekana kuwa kubwa zaidi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ikilinganishwa na wahasimu wao Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema).

Tangu kampeni hizo zizinduliwe takribani wiki moja iliyopita mtandao huu umekuwa ukizifuatilia kampeni hizo kwa jirani na hiyo ndiyo picha inayodhihiri.

Ukiachilia mbali baadhi ya viongozi na timu zao za kampeni ambao wanatoka nje ya kata hiyo, idadi kubwa ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo wanaishi katika kata hiyo jambo linaloashiria mwamko mkubwa wa wapiga kura wa kata hiyo kujitokeza kuwasikiliza wagombea wa vyama hivyo, ahadi zao na za vyama vyao.

Wakati CCM imemsimamisha Baraka Kimata, diwani wa zamani wa kata hiyo kupitia Chadema; Chedema wamemsimasha Bahati Chengula.

Zikiwa zimebaki takribani wiki mbili kufanyika kwa uchaguzi huo, kila chama kimekuwa kikijinasibu kushinda uchaguzi huo mdogo.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment