Thursday, 26 October 2017

SUGU APINGA MAGAZETI KUFUNGIWA

Image result for sUGU

Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ameitaka Serikali kuacha mwenendo wa kutisha, kushambulia na kudhibiti vyombo, waandishi na uhuru wa habari.

Ametoa kauli hiyo baada ya Serikali kulifungia kwa siku 90 gazeti la kila siku la Tanzania Daima.

Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema amesema kulifungia gazeti hilo ni vitisho na mashambulizi dhidi ya uhuru wa habari na vyombo vya habari.

Amesema hali hiyo ikiachwa iendelee bila kukemewa na kupingwa itazidisha sitofahamu.

Waziri huyo kivuli amesema uamuzi huo wa Serikali ni kinyume cha misingi ya utoaji haki, kwa maana ya kuwa mlalamikaji, kukamata, kufungua mashtaka, kuendesha mashtaka na kuwa hakimu au jaji wa kesi yake yenyewe.


“Hii haikubaliki katika misingi ya utawala bora unaozingatia sheria,” amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment